Monday, April 27, 2015

About Beyonce

Beyoncé Giselle Knowles (alizaliwa 4
Septemba 1981 ), anayefahamika zaidi kwa jina
moja Beyoncé ni
mwimbaji wa R & B, mtunzi wa nyimbo,
mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji na
mwanamitindo kutoka Marekani. Alizaliwa na
kukulia Houston, Texas na alihudhuria shule
mbalimbali zinazofunza sanaa. Pia alianza
kushiriki katika mashindano ya kuimba na
kucheza ngoma akiwa mtoto. Knowles alikuja
kujulikana katika mwisho wa miaka ya 1990
kama mwimbaji kiongozi wa kikundi cha
wasichana cha R & B, Destiny's Child .
Kulingana na Sony , mauzo ya rekodi za
Knowles, yakiunganishwa na yale ya kikundi
cha Destiny's Child, yamezidi milioni 100.

Wakati wa kuvunjika kwa kikundi cha
Destiny's Child , Knowles alitoa albamu yake
ya kwanza, Dangerously in Love (2003),
ambayo ilikuwa mojawapo ya albamu za
mwaka zilizokuwa na mafanikio zaidi na jambo
hili liliashiria uwezo wake wa kufaulu kama
msanii kivyake. Albamu hiyo ilikuwa na
mafanikio muhimu ya kibiashara, huku ikitoa
nyimbo mashuhuri kama " Crazy in Love ",
" Baby Boy ", na kumshindia Knowles tuzo tano
za Grammy katika mwaka 2004 . Kutawanyika
kwa kikundi cha Destiny's Child mwaka 2005
kuliendeleza mafanikio yake: albamu yake ya
pili, B'Day , iliyotolewa mwaka 2006, ilikuwa
namba moja kwenye chati za Bango , na
ilikuwa na nyimbo kama " Déjà Vu ",
" Irreplaceable ", na " Beautiful Liar ". Albamu
yake ya tatu, I Am... Sasha Fierce, ilitolewa
Novemba 2008, na ilikuwa na nyimbo kama " If
I Were a Boy", " Single Ladies (Put a Ring on
It) ", " Halo" na " Sweet Dreams ". Knowles
amefikisha idadi ya nyimbo tano zinazopendwa
sana miongoni mwa orodha ya nyimbo 100,
hivyo basi kuwa mmoja kati ya wasanii wawili
wa kike walio na idadi kubwa ya nyimbo
zilizochukua nafasi ya kwanza katika miaka ya
2000.

Mafanikio ya albamu alizoimba akiwa peke
yake yamemfanya Knowles kuwa mmoja wa
wasanii wanaosifika sana katika sekta ya
muziki, na amepanua kazi yake kwa
kujihusisha na uigizaji na kuidhinisha bidhaa.
Alianza kazi yake ya uigizaji mwaka 2001,
aliposhiriki katika filamu ya kimuziki [4] Katika
mwaka wa 2006, alishiriki kama mmoja wa
wahusika wakuu katika filamu ya malinganisho
ya 1981 ya Broadway musical Dreamgirls,
ambayo ilimfanya ilimpatia uteuzi mara mbili
katika Golden Globe Nominations . Knowles
alizindua shirika la familia yake la mitindo,
House of Deréon, mwaka 2004, na limekuwa
likihusika na kuidhinisha bidhaa kama Pepsi,
Tommy Hilfiger , Armani na L'Oréal . Katika
mwaka wa 2009, jarida la Forbes
lilimworodhesha Knowles namba nne katika
orodha yake ya watu mashuhuri walio na
nguvu na ushawishi mkubwa katika dunia, wa
tatu katika orodha ya wanamuziki wa hadhi ya
juu, na namba moja katika orodha ya juu ya
watu mashuhuri wanaolipwa malipo bora zaidi
chini ya miaka 30, akiwa na zaidi ya mapato
ya dola milioni 87, kati ya 2008 na 2009.

Maisha na kazi mwanzo

Knowles alizaliwa katika Houston , Texas, na ni
binti wa Mathew Knowles , meneja mashuhuri
wa rekodi, na Tina Beyincé, mtengenezaji wa
mavazi na nywele. Babake Knowles 'ni
Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika na mama
yake ni Mkrioli mwenye asili ya (Mwafrika
Mmarekani, Mmarekani alisia, na Mfaransa). [4]
Knowles alibatizwa na kuchukua jina la mama
yake la kati, kama ishara ya shukrani kwa
mama yake na kuzuia jina hilo lisisahaulike,
kwani ni wanaume wachache tu wa familia ya
Beyincé wanaolitumia jina hilo. [4] Babu na bibi
wa mama yake, Lumis Albert Beyincé na Agnéz
Deréon, walikuwa Wakrioli kutoka
Louisiana.waliozungumza Kifaransa [4] Yeye ni
dada mkubwa wa Solange , mwimbaji - mtunzi
wa nyimbo, na mwigizaji.
Knowles alisomea St Mary's Elementary
School katika Texas, ambapo yeye alihudhuria
madarasa ya kucheza dansi, ikiwa ni pamoja
na ballet na jazz. Kipawa chake cha kuimba
kiligunduliwa wakati mwalimu wake wa dansi
alipoanza kuimba wimbo na yeye akaumaliza
wimbo huo, na kuweza kuimba noti za juu. [5]
Ingawa alikuwa msichana mwenye soni, kama
mama yake alivyosema, upendo wa Knowles
wa kuimba na kucheza muziki ulianza bila
kutarajiwa baada ya kushiriki katika shindano
la kuonyesha vipawa shuleni. Mara tu
alipopata nafasi ya kupanda jukwaani, yeye
aliweza kukabiliana na soni zake na akataka
kuwa mwimbaji na mchezaji dansi.[6] Akiwa
na umri wa miaka saba, Knowles aliingia
shindano lake la kwanza la kuonyesha kipawa
chake, na kuimba wimbo wa John Lennon ,
"Imagine". Yeye alishinda na akapongezwa
kwa shangwe na vifijo. [7][8] Akiwa na umri
huo, Knowles alianza kuwavutia waandishi wa
habari, alipotajwa katika Houston Chronicle
kama mmoja wa walioteuliwa kushindana
katika maonyesho ya mtaani ya 'The Sammy'.

Mnamo 1990, Knowles alijiunga na Parker
Elementary School, shule inayofunza muziki
huko Houston, ambapo alikuwa akiimba katika
kwaya ya shule. [5] Pia alihudhuria shule ya
The High School for Performing and Visual Arts
katika Houston [10] na baadaye akaenda Alief
Elsik High School , iliyo katika eneo la Houston
la Alief. [4][11] Knowles alikuwa kiongozi wa
nyimbo katika kwaya ya kanisa lake, la St
John's United Methodist. [5] Hata hivyo, yeye
alikaa katika kwaya kwa miaka miwili kwa
sababu alikuwa anashughulikia kazi yake ya
muziki. [12]
Akiwa na umri wa miaka minane, Knowles
alikutana na LaTavia Roberson akiwa katika
majaribio ya kikundi cha waimbaji wasichana.
[13] Wao, pamoja na rafiki ya Knowles Kelly
Rowland , waliwekwa katika kikundi kilichoimba
rap na kucheza dansi. Mwanzoni kikundi hiki
kilichoitwa Girl's tyme , [7] kilipunguzwa na
kuwa cha wasichana sita. [5] Kutokana na
kuwepo kwa Knowles na Rowland, kikundi hiki
cha Girl's tyme kiliwavutia watazamaji katika
taifa zima. Mtayarishaji wa R&B kutoka pwani
ya magharibi, Arne Frager, alisafiri kwa ndege
hadi Houston ili kuwaona. Hatimaye yeye
aliwapeleka kwenye studio yake - The Plant
Recording Studios - iliyoko Kaskazini mwa
California , na kushirikisha nyimbo za Knowles
kwa sababu yeye ,Frager, alifikiria kuwa
Knowles alikuwa na uwezo wa kuimba. [5]
Kama sehemu ya jitihada za kuingiza kikundi
cha Girl's tyme kwenye studio kubwa ya
kurekodi, mkakati ambao Frager alipanga
kuutumia ulikuwa ni kwanza kukishirikisha
kikundi hiki katika Star Search, [6] kipindi
kilichokuwa kikubwa zaidi cha kuonyesha
kipawa kwenye TV ya kitaifa kwa wakati ule.
[5] Girl's tyme walishiriki katika mashindano
lakini wakashindwa kwa sababu wimbo
waliouimba haukuwa mzuri, Knowles
mwenyewe alikubali. [14][15] Knowles alipatwa
na "kipingamizi " cha kwanza katika kazi yake
baada ya kushindwa, lakini baada ya
kugundua kuwa waimbaji wengine mashuhuri
kama Britney Spears na Justin Timberlake
walipitia kipingamizi kama kile, yeye alirejesha
tumaini. [5]
Ili kusimamia kikundi hiki, babake Knowles
(ambaye wakati huo alikuwa muuzaji wa vifaa
vya matibabu) alijiuzulu katika mwaka wa
1995 kutoka kwa kazi yake. [16] Yeye kujitolea
muda wake na kuanzisha kambi ya "Boot
Camp" kwa ajili ya mazoezi yao. [6] Hatua hii
ilipunguza pato la familia ya Knowles kwa
nusu na wazazi wake wakatengana kwa
sababu ya shinikizo iliyotokana na hatua hiyo
ya kujiuzulu. [4] Muda mfupi baada ya
kuingizwa kwa Rowland, Mathew alipunguza
idadi ya awali ya kikundi hiki hadi nne, [5] na
LeToya Luckett aliyejiunga nao katika mwaka
wa 1993. [13] Huku wakifanyia mazoezi katika
chumba cha Tina cha kutengenezea nywele na
kwenye vitaru vya nyumba zao, kikundi
kiliendelea kuimba kama katika maonyesho ya
vikundi vingine vya wasichana vya R&B
vilivyokuwa tayari vimefahamika; [13] Tina
alichangia kwa kutengeneza mavazi yao, jambo
ambalo aliendelea kufanya hata katika wakati
wa kikundi cha Destiny's Child. Pamoja na
msaada wa Mathew, wao walifanyiwa
majaribio ya sauti na kampuni za kurekodi na
hatimaye wakasainiwa na kampuni ya Elektra
Records, ambayo iliwafutilia mbali baada ya
miezi michache kabla hawajatoa albamu
yoyote.

Thursday, October 23, 2014

Jay Z na Beyonce wakumbushia viapo vyao vya ndoa

Beyoncé na Jay Z wameamua kuzizika kabisa
tetesi za kuwa ndoa yao imekufa kwa
kukumbushia viapo vyao vya ndoa.. ama kwa
lugha rahisi kufunga ndoa tena.

Kwa mujibu wa jarida la People, mastaa hao
waliosherehekea miaka sita ya ndoa yao mwezi
April, hivi karibuni walifunga ndoa tena.
“Walikuwa na matatizo makubwa,” chanzo kimoja
kimeliambia jarida hilo.. “Lakini walimaliza na
kuamua kufunga ndoa tena.”

New Music: Mwana FA Ft Ally Kiba-Kiboko Yangi

<img href="http://www.hulkshare.com/2k6zmrj3qbog"> DOWNLOAD HERE">